MWANAMKE:
KWANINI UWE NA MZUNGUKO MBOVU WA HEDHI? VISABABISHI NA SULUHU IKO HAPA.
Imekua kawaida kuwasikia Wanawake wakilalamikia kuhusiana na mizunguko Mibovu ya hedhi ambayo imekua ikiambatana na maumivu makali ya tumbo la chini,
*kuingia hedhi mara mbili kwa mwezi
*Kutokwa damu nyingi na kwa kipindi kirefu.
Leo tutaangalia visababishi vya matatizo hayo pamoja na suluhisho lake ambalo litakuweka wewe binti/Mwanamke/mama ufurahie siku zako za hedhi na sio kuzichukia
SABABU ZA KUWA NA MZUNGUKO MBOVU/UNAOBADILIKA MARA KWA MARA;
>MAZINGIRA
Mazingira yanaweza kumfanya Mwanamke kuwa na mzunguko usioeleweka. Kuhama kutoka kwenye eneo lenye baridi kwenda eneo lenye joto inaweza kusababisha hali hiyo.
>Kuwa na hofu/uoga/stress
>Uwepo wa uvimbe kwenye kizazi
>Matatizo ya mfumo wa homoni #hili ndio tatizo kuu kwa akina dada hasa kutokana na vyakula wanavyopenda kuvitumia
>Matatizo katika vifuko vya mayai na tabaka la ndani la kizazi
>Maambukizi sugu katika kizazi,
Maranyingi unapoenda hospital unaambiwa una U.T.I , lakini ukweli sio hivyo
>Kutokwa na uchafu ukeni na maumivu wakati wa tendo la ndoa ambayo hupelekea Mwanamke kutofurahia tendo la ndoa.
Uchunguzi hufanyika katika kliniki za magonjwa ya akina mama ambapo vipimo mbalimbali hufanyika ikiwemo vipimo vya damu,Mkojo,Ultrasound na vingine.
ATHARI ZA MZUNGUKO USIOELEWEKA:
Sio suala la kufurahia kuishia kusikitika unapokuwa na tatizo. Madhara yake ni kama ifuatavyo;
1.Kutopata UJAUZITO
2. Maambukizi katika via vya uzazi
3. Kuziba kwa mirija ya uzazi
4. Kupoteza hamu ya tendo la ndoa ikiwa ni pamoja na kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
Comments
Post a Comment