MAAJABU YA MAJI KATIKA MATIBABU




Kupona Bila Dawa


Miili  yetu ina njia mbalimbali za kujikinga dhidi ya maradhi yanayoweza kutupata, njia hizi ni bora zaidi kuliko kutumia dawa. Magonjwa mengi huitaji kinga zaidi sio tiba. Magonjwa kama vile mafua, flu nakadhalika.
Ili kusaidia mwili kujikinga na maradhi ni lazima mtu aweze kujimudu kwa mambo yafuatayo:

Kujiweka katika hali ya usafi wakati wote
Kula chakula bora
Kupata muda  wakutosha kupumzika/kupumzisha mwili.
Hata kama ugonjwa ni wa kutisha na unahitaji dawa, mwili ndio unapambana na ugonjwa dawa zinasaidia tu. Jambo la muhimu kuzingatia ni usafi, kupumzika na kula chakula bora.

Huduma za kiafya hazitegemei dawa, hata kama unaishi sehemu ambazo hazina dawa za kigeni kuna mambo mengi unayowza kufanya ili kukinga na kutibu magonjwa mengi, kinachotakiwa ni uelewa tu wa namna  ya kufanya.

Je, kuna magonjwa yanayoweza kukingwa na kutibiwa bila  kutumia dawa?
Kama  watu wanaelewa namna nzuri ya kutumia maji basi hii itakuwa namna nzuri ya kukinga na kuponyesha magonjwa bila kutumia dawa.

Watu wengi  tunaishi bila  kutumia dawa lakini kati  yetu hakuna hata  mmoja anayeweza kuishi bila maji. Ukweli ni  kwamba zaidi ya 57% ya mwili wa mwanadamu ni maji. Kama mtu anayeishi kijijini angeweza kutumia  maji vizuri basi magonjwa na vifo hasa watoto wadogo yangepungua sana.
Matumizi mazuri ya maji ni msingi wa kuzuia na kutibu ugonjwa wa kuharisha. Kuharisha ni ugonjwa mkubwa unaosababisha vifo kwa watoto wadogo katika sehemu nyingi ulimwenguni, maji machafu ndio  husababisha ugonjwa  huu.

Njia mojawapo ya kuepuka ugonjwa huu wakuarisha ni kuchemsha maji ya kunywa na kupikia hasa kwa watoto wadogo(wachanga). Chupa  ya maziwa na vyombo vingine vya mtoto mchanga vinatakiwa vichemshwe kabla na baada ya kutumiwa. Kuosha  mikono kwa sabuni baada ya kutoka  msalani na kabla  ya kula chakula.

Ukosefu wa maji mwilini ni sababu  kubwa ya vifo kwa  watoto wenye ugonjwa wa kuharisha. Kama mtoto anapewa maji mengi yaliyo na chumvi  na sukari au asali kidogo hii itakinga na hata kutibu  upungufu wa  maji mwilini. Kumpa mtoto mwenye kuharisha maji mengi itamfaa zaidi kuliko dawa. Ukweli  ni kuwa unapompa mtoto maji ya kutosha huitaji kumpa dawa yoyote ya kutibu kuharisha.

Je, ni nyakati  gani ambapo mtumizi ya maji yanafaa zaidi kuliko dawa?
Unapougua magonjwa  kama;
Kuhara, minyoo na ugonjwa wa tumbo
Vidonda vyenye usaha, pepopunda
Magonjwa ya ngozi

Ukiugua ugonjwa wa ngozi{oga kila siku}
Kila mara kwa  nawa mikono yako na sabuni wakati wa kuamka asubuhi, baada ya kutoka haja kubwa au ndogo na kabla ya kula chakula.

Oga mara kwa mara.
Kila siku wakati hali ya hewa ni joto, oga baada ya kazi ngumu au baada ya kutokwa na jasho. Kuoga mara kwa mara kunasaidia kukinga maradhi ya ngozi, mba, chunusi, kuwashwa na vipele. Wagonjwa pamoja na watoto wadogo ni lazima waogeshwe kila siku.

Uvaaji wa viatu.
Katika sehemu ambazo kuna safura, usitembee bila viatu na usiwaruhusu watoto kufanya hivyo. Kwa kuwa minyoo huingia mwilini kwa kutoboa nyayo za miguu, kwa kawaida minyoo ya safura haiwezi kuonekana kwenye choo. Hivyo kipimo ni cha laazima ili kuhakikisha minyoo hao wapo au la!.

JINSI SAFURA INAVYOENEZWA
Safura wachanga humwingia mtu kwa kutoboa kwenye nyayo za miguu iliyokuwa na viatu, hii inaweza kusababisha muwasho kwenye miguu.

Baada ya siku chache hufika kwenye mapafu kwa kupitia kwenye damu, wanaweza kusababisha kikohozi kikavu(mara chache mgonjwa hukohoa damu)
Mtu hukohoa hawa safura wachanga na kuwameza

Siku chache baadaye mtu anaweza kuharisha au kuumwa tumbo
Safura hujishikiza kwenye kuta za tumbo. Safura wengi husababisha ulegevu na upungufu wa damu mwilini.

Mayai ya safura hutoka mwilini yakiwa yamechanganyikana  kwenye choo cha mgonjwa. Mayai hayo huanguliwa yakiwa kwenye udongo wenye majimaji.
Tanbihi;ugonjwa wa safura unaweza kuwa mojawapo ya magonjwa hatari zaidi kwa watoto. mototo yeyote mwenye upungufu wa damu, mweupe sana na anayekula uchafu anaweza kuwa na safura. Ikiwezekana choo chake lazima kipimwe.

MATIBABU YA SAFURA
Tumia;
Thiabendazole(mintezol)
Mebendazole
Tetracholoroethylene(TCE) au
Bephenium(alcopar) kwa kipimo na tahadhari
Tanbihi; Tibu upungufu wa damu kwa kula vyakula vyenye madini ya chuma kwa wingi na tumia vidonge vyenye madini ya chuma kwa wingi.

Zingatia usafi wa kinywa.
Piga meno yako mswaki kila siku na kila baada ya kula . Ikiwa huna mswaki au dawa ya meno sugua meno yako na chumvi pamoja na hamira.

Ikiwa huna mswaki;
Tumia tawi la mti, chonga upande mmoja uwe mkali ili kusukutua katikati ya meno. Na upande mwingine uwe kama nyuzinyuzi za mswaki.
Ikiwa huna dawa;
Tengeneza poda ya meno kwa kuchanganya chumvi na magadi katika sehemu zilizo sawa. Ili kuifanya ikae kwenye mswaki, loweka mswaki huo kwenye maji kabla ya kutumbukiza kwenye poda. chumvi pamoja na magadi soda hufanya kazi sawa sawa na dawa ya meno kwa kusukutulia meno, kama huna magadi tumia chumvi yenyewe tu.

Ikiwa jino lina shimo.
Ili kuzuia jino lisilete maumivu zaidi au lisilete jipu, epuka vitu vitamu na sukutua vizuri kila baada ya kula. Ikiwezekana muone mtaalamu wa meno mara moja. Kama ukiweza kumuona mapema anaweza kusafisha na kuliziba jino lako kitu ambacho kitalifanya likae muda mrefu bila tabu yoyote.

Tanbihi: unapokua na jino lenye shimo au limeoza, usingoje mpaka liume sana. Nenda kwa mtaalamu wa meno mara moja likazibwe.
Jinsi ya kutibu vidonda vyenye usaha

*kutibu jeraha;
Osha kwanza mikono yako vizuri ukitumia sabuni na maji safi.
Osha jeraha vizuri ukitumia maji ya moto
Unaposafisha jeraha hakikisha uchafu wote unatoka. Hakikisha kuwa chini ya ngozi iliyojeruhiwa kumesafishwa pia.
Kama inawezekana mwagia maji ya moto kwenye jeraha kwa kutumia sindano.*Uchafu wowote utakaobaki unaweza kusababisha ugonjwa
Itaendelea...........
Kwa maoni na ushauri niandikie:
                  Email:chindindindi88@gmail.com
Simu:0659159726

Comments

Popular Posts