JINSI UNAVYOWEZA KUPATA MTAJI WA BIASHARA/UJASIRIAMALI



JINSI UNAVYOWEZA KUPATA MTAJI WA BIASHARA/UJASIRIAMALI

Upatikanaji wa mitaji kwa nchi zinazoendelea kama Tanzanian ni kilio cha wengi kwa walio katika Ujasiriamali au wenye nia ya kuingia kwenye Ujasiriamali hususani vijana waliohitimu vyuo vikuu na wale ambao hawakubahatika kuendelea na elimu ya juu. Wengi hulia watapata wapi mtaji wa kuanzisha biashara au kwa wale waliothubutu kuanza watawezaje kuendeleza biashara zao, ingawa taasisi za kifedha zimekua mstari wa mbele kwa utoaji wa mikopo mbalimbali ya fedha au pembejeo kwa viwangk tofauti kilingana na uhitaji uliopo kwaajili ya kuanzisha au kukuza na kuendeleza  biashara kwa wajasiriamali.
Ni muhimu Mjasiriamali kujua vyanzo mbalimbali vya mitaji, upatikanaji wake na gharama zake pia kujua ni kiasi gani cha mkopo unaohitaji muda wa kurejesha mkopo na riba  ili uweze kuchagua chanzo sahihi cha mtaji unaohitaji na unaoendana na biashara yako kwa gharama nafuu(riba ndogo).
MTAJI NI NINI?
Ni kitu chochote ambacho unaweza kutumia kuzalisha kitu kingine kwa lengo la kupata faida. Mtaji kwa lugha rahisi ni KIANZIO cha biashara. Kwa mfano mtaji wa Maman'tilie ni :-
Jiko, mwiko, sufuria, sahani, maji pamoja na fedha kwaajili ya kununulia chakula kama: Michele, chumvi, maharage, nyanya pamoja na viungo vingine. Hii ni kwasababu biashara yoyote lazima iwe na mtaji ili kununua malighafi kwaajili ya kudumisha biashara zao. Mtaji sio pesa pekee kama wengi tunavyodhani.
AINA ZA MITAJI:
Fedha
Akili(ubunifu)
Watu
Bidhaa au vifaa vya kuzalishia bidhaa(to a mfano)
Fedha, hizi huweza kuzalisha mapato au kwa kuwekeza katika biashara au Mali ili kupata mapato. Fedha zinaweza kutumika katika biashara kununua au kumlipia vitu vinavyohitajika katika kuendesha biashara zao au kutoa huduma zao kwa lengo la kupata faida.
AKILI(ubunifu), Akili au ubunifu wako unaweza kuwa ndio mtaji pekee hasa katika kazi zinazohitaji utaalamu zaidi mfano, kubuni na kuanzisha biashara fulani sehemu fulani inayorndana na eneo hilo ambayo haijawai kufanya na mtu katika eneo hilo, hivyo mtaji hutegemea aina ya biashara ambayo mtu anataka kufanya.
WATU, mtaji huu umegawanyika katika sehemu mbili moja ni ujuzi, kipaji, maarifa, tabia, ubunifu na utambuzi wa mambo katika Uwezo wa kufanya kazi ili kuzalisha thamani za kiuchumi. Mtaji huu huwa unaandaliwa na muhusika mwenyewe kwa kusoma, kufanya shughuli fulani na kupata ujuzi ambao utamuwezesha kukubalika katika jamii na kumuingizia kipato na kumpatia utajiri yeye mwenyewe au familia.
Kwa leo tuishie hapa tutaendelea kuangalia vyanzo vya mitaji katika makala ijayo.........

Comments

Popular Posts