GHARAMA YA MABADILIKO KATIKA UJASIRIAMALI
GHARAMA YA MABADILIKO
Hakuna kitu chochote duniani kilichotokea chenyewe bila msukumo wa aina yoyote iwe kisiasa,kiuchumi,kijamii au kiutamaduni lazima kuna nguvu iliyotumika watu walijitoa ili kuhakikisha wanafikia mabadiliko waliyokusudia. Kitu chochote ili kiweze kuhama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine lazima kuna nguvu imetumika kuhamisha kitu hicho, hivyo unapozungumzia gharama ya mabadiliko maana yake ni kujitoa katika kufanikisha jambo unalokusudia kulifanya kwa ufanisi. Gharama yaweza kuwa nguvu kazi,mtaji,kufuata ushauri wa kitaalamu, kutenga muda wa kutosha katika kufanikisha shughuli unayokusudia kuifanya, waswahili husema “Punda afe mzigo ufike” maana yake ni kwamba jua liwake mvua inyeshe lazima safari ya kutafuta maendeleo itimie.
Maisha sio tukio la ajali, hakuna taifa lolote duniani lililofanikiwa kwa bahati mbaya inachukua miongo mingi kuweza kufikia mafanikio tunayoyaona, mfano mzuri taifa la Marekani unaloliona hivi sasa halikua hivyo miaka mia moja iliyopita kipindi cha akina Abraham Lincoln. Kuna watu waligharamia ujenzi wa taifa hilo na kuweka misingi imara iliyowawezesha kufikia hapo walipo hivi sasa. Hivyo ili uweze kuwa na maendeleo endelevu lazima kwanza ukubali kugharamia maendeleo hayo.
Binadamu alikuja duniani akiwa hana kitu chochote, vyote tuvionavyo ni juhudi za binadamu hao hao katika kuhakikisha wanaendana na mabadiliko yanayojitokeza katika maisha yao ya kila siku katika nyanja zote kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.
Kumfundisha mtu jinsi ya kuvua samaki ndio njia pekee ya kumsaidia mtu huyo kuondokana na maisha ya kuwa tegemezi katika maisha yake yote. Sasa ni wakati ambao unatakiwa ujitambue kuwa wewe ni nani, nini unatakiwa kufanya ili kuweza kuondokana na hali uliyonayo sasa kwenda hatua nyingine itakayo kufanya wewe kuwa chachu ya maendeleo kwa kujitoa kwako.
Wale wote waliotayari kujitoa na kutumia fursa zinazo wazunguka ndio wenye nafasi kubwa ya kufanikiwa katika ulimwengu huu “Umaskini ni idadi ya fursa ulizopoteza na utajiri ni idadi ya fursa ulizo zitumia vema’’ askofu Josephat Gwajima. Mabadiliko makubwa huhitaji msukumo mkubwa kutoka ndani ‘applied force’ kuweza kufikia malengo uliyojiwekea.
Lakini pia, katika kila juhudi unayofaya Kufikia malego kuna nguvu nyingine hufanya kazi ya kukurudisha nyuma, nguvu hiyo yaweza kuwa ya ndani au nje. Waswahili husema “filimbi nyingi humpoteza mbwa’’. Hutakiwi kugeuka na kuwatazama waache waendele kukutazama utakapofika maana hawawezi kuzuia kusudi la Mungu kwako.
Mabadiliko huendana na muda lakini muda peke yake hauwezi ukabadili chochote. Kwa mfano mtu aliye feli mtihani miaka 15 iliyopita itamchukua muda gani kubadili matokeo na kuwa mazuri kama alikaa tu bila kufanya chochote kwa kipindi hicho chote?. Itamhitaji atumie muda mrefu kujiandaa kitu kinacho washinda wengi. Njia pekee inayoweza kumsaidia kupata matokeo mazuri ni kujisajiri kwaajili ya kufanya mtihani, kupitia maandalizi yake na kuyafanyia marekebisho, kutafuta msaada kupitia vitabu na watu mbalimbali waliomtangulia ndipo arudie mtihani. mabadiliko hayo huweza kuonekana ndani ya mwaka mmoja, hivyo hakuna sababu ya kukaa na kuendelea kuamini kwamba wewe ni wa kufeli tu. Kusubiri mabadiliko bila kuonesha juhudi za kutaka kuyabadili maisha ni sawa na kupaka rangi upepo. Ukijua unachokifanya na ukakifanya kwa kujitoa lazima utapata matokeo mazuri katika shughuli unayoifanya, hivyo hakuna mafanikio yasiyo na gharama.
Gharama ya mtaji wa Mabadiliko
Nidhamu ni silaha muhimu sana katika maisha, nidhamu ni mwanga na silaha ya mafanikio kwani hukufanya uweze kukubalika na jamii na kukujengea heshima kubwa katika jamii inayo kuzunguka, kwa kufanya hivyo utaweza kuaminika na kila mmoja. Mtu akiuliza nidhamu ni nini?. Jibu kwa ufupi, nidhamu ni kutambua wajibu wako katika jamii. Je, kutambua wajibu pekee ndio nidhamu?. Jibu ni hapana nidhamu ni kutambua na kutekeleza wajibu wako kwa jamii na Taifa kwa ujumla. Mwingine akasema “hutoshindwa isipokua kwa kuwatazama na kuwafuata wanao kutazama na kukukatisha tamaa’’.
Kila wakati usipende kuwanyooshea wengine kidole kuwa ndio chanzo cha matatizo uliyonayo au kushindwa kwako, kumbuka unapo nyoosha kidole kimoja kwa wengine kuwa ndio chanzo cha matatizo yako, vidole vitatu vinakunyooshea wewe na kimoja kinamuonesha Mungu kama shahidi wa hicho unachokifanya. Hii ina maana kwamba kila mtu ni mhusika kwa 75% wa matatizo aliyonayo, kama kuna mtu anahusika basi ni 25% tu za kumlaumu mtu huyo, hii inamaana kwamba kushinda au kushindwa hutokana na juhudi zako mwenyewe, ukishindwa ni jitihada zako, ukifanikiwa pia ni jitihada zako.
Wanao amini katika mafanikio siku zote huonesha jitihada kwa kile wanachokifanya ili wapate mabadliko/mafanikio wanayohitaji kufikia(kuishi ndoto zao) Someone said “stubbornness and an unwillingness to change is the energy of fools’’.
Mafanikio/mabadiliko ni gharama. Hii ina maana kuongeza thamani na kuongeza thamani kunahitaji gharama. Kwa mfano; badala ya kuuza mahindi kilogramu 50 kwa shilingi za kitanzania 5,000/= unatengeneza unga wa sembe na kuuza kwa shilingi za kitanzania 100,000/= au badala ya kuuza machungwa mkulima atatengeneza juisi ambayo itamuingizia fedha nyingi kuliko angeuza machungwa. Mahatma Gandhi aliwai kusema “tunatakiwa kupambana kusudi tuweze kufikia mabadiliko tunayo hitaji kuyaona’’. Je, ni kweli unahitaji mafanikio?, uko tayari kufanikiwa kama waliokutangulia?. Kama jibu ni ndio huu ndio muda wa kufanya maamuzi sahihi bila kuangalia umeanguka mara ngapi?. Acha kutengeneza visingizio.
“Anyone who will move the world,must first move himself’’ yeyote atakaye ibadilisha dunia lazima/sharti abadilike yeye kwanza. Maneno ya Socrate.
Endelea kufuatilia makala mbalimbali za Hamasa na Ujasiriamali kupitia blog yako ya
zemwalimu.blogspot. com

Comments
Post a Comment